Tangaza Hapa Ad

Michezo

VIDEO: Man United imelazimishwa sare Mourinho akitolewa katika benchi

on

Klabu ya Machester United ya England November 27 2016 imecheza dhidi ya West Ham United katika uwanja wake wa Old Trafford na kulazimishwa sare ya kufungana goli 1-1.

3acd9f0e00000578-0-image-a-128_1480266048325

West Ham United ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 2 kupitia kwa Diafra Sakho, lakini Zlatan Ibrahimovic aliisawazishia Man United goli dakika ya 21 ya mchezo.

screen-shot-2016-11-27-at-10-07-48-pm

Hata hivyo mchezo huo uliyomalizika kwa sare ya goli 1-1, umemalizika kwa kocha wa Man United Jose Mourinho kutolewa katika benchi na kwenda jukwaani kutokana na kupiga chupa ya maji kwa hasira, huku Paul Pogba akioneshwa kadi ya tano ya njano itakayomfanya akose mchezo ujao.

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement