Tangaza Hapa Ad

Michezo

Mourinho kajibu kwa nini alimuacha Herrera vs Basel

on

Kocha wa Man United Jose Mourinho ambaye usiku wa September 12 2017 aliiongoza Man United katika mchezo wa UEFA Champions League dhidi ya Basel na kufanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-0, ameamua kuweka wazi kwa nini hakumtumia Ander Herrera.

Ander Herrera alicheza game yake ya kwanza ya msimu wa Ligi Kuu England weekend iliyomalizika Man United ikiambulia sare ya 2-2 dhidi ya Stoke City lakini kiungo huyo aliachwa katika mchezo wa jana wa Champions League dhidi ya Basel.

Pogba

Jose Mourinho ameweka wazi kuwa maamuzi yake hayo yalikuwa ya kiufundi wala hakuna sababu nyingine kwa sababu aliamua kutumia viungo wawili Matic, Pogba na Herrera kumuacha.

Herrera

“Hakuna sababu za ziada kwa Herrera kuwa nje, game ambayo tuliamua kutumia viungo watatu Herrera alicheza lakini tulitumia viungo wawili tu Matic na Pogba na walicheza vizuri hivyo hatukuona sababu ya kufanya mabadiliko, hata hivyo Fellaini na Carrick walikuwepo benchi pia ” >>> Jose Mourinho

Video ya dakika 3 ya magoli ya Taifa Stars vs Botswana September 1 2017, Full Time 2-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement