Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

UTANI: “Poleni wabongo tumefunga nyinyi na shemeji yenu Zari”

on

Ijumaa ya December 15 2017 timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes ilifanikiwa kuingia katika historia nyingine baada ya kufanikiwa kuwatoa Mabingwa kihistoria wa michuano ya CECAFA Senior Challenge Cup timu ya taifa ya Uganda The Cranes katika michuano hiyo.

Uganda wametolewa katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya CECAFA Senior Challenge Cup kwa kufungwa kwa magoli 2-1, hivyo kwa ushindi huo sasa Zanzibar watacheza mchezo wa fainali ya michuano hiyo dhidi ya wenyeji wa michuano hiyo timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars.

Haji Manara

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Zanzibar waliifunga pia Tanzania bara yaani Kilimanjaro Stars kwa magoli 2-1 katika hatua ya makundi, hivyo baada ya ushindi wa leo wa Zanzibar utani umeanza kusambaa mtandaoni unaosema eti “Znz 2-1 Uganda mpira kipaji pole wabongo tumewafunga nyinyi na shemeji yenu zari”

Afisa habari wa Simba Haji Manara akapost ujumbe huo unaosambaa mtandaoni kwa utani pia halafu akaandika “Wazanzibar mtatuua kwa hyo maneno yenu jamani…kwa hyo huku Bara wote shem letu ni @zarithebosslady ? haya bana,Cc twaendelea kuwaombea dua @diamondplatnumz @emmanuelokwi ??”

UTANI: Haji Manara kwa wapinzani wao Yanga baada ya Simba kumpata MO Dewji

Soma na hizi

Tupia Comments