Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Man City imevunja rekodi ya Man United Old Trafford leo

on

Baada ya mashabiki wa soka kusubiri kwa hamu mchezo wa watani wa jadi wa Man United dhidi ya Man City katika uwanja wa Old Trafford ili kufahamu kati ya Manchester United na Man City ni timu gani itavunja rekodi ya mwenzake leo.

Kabla ya game ya leo Man United walikuwa hajafungwa kwa game 40 katika uwanja wao wa nyumbani wakati Man City walikuwa wamepata ushindi katika game 13 mfululizo katika michezo ya Ligi Kuu England msimu wa 2017/2018, hivyo Man City wamepata ushindi wa 14 EPL mfululizo.

Man City ya Pep Guardiola imefanikiwa kuvunja rekodi ya Man Unired ya Mourinho baada ya kuifunga kwa magoli 2-1, magoli ya Man City yakifungwa na David Silva dakika ya 43 na Otamendi dakika ya 54 wakati goli pekee la Man United likifungwa na Marcus Rashford dakika za nyongeza kipindi cha kwanza.

VIDEO: Atayofanya Mo Dewji kwa Simba ndani ya mwaka mmoja

Soma na hizi

Tupia Comments