Biko


Tangaza Hapa Ad

Burudani

Nelly amejibu kuhusu tuhuma za kudaiwa kubaka

on

Baada ya msanii kutokea nchini Marekani “Nelly” mwenye umri wa miaka 42 aliyetuhumiwa kwa mashitaka ya kumbaka mwanamke mmoja huko jijini Washington na kufunguliwa mashtaka October 7 2017 ameweka wazi kuhusu kinachoendelea.

Inadaiwa kuwa mwanamke huyo aliwapigia simu polisi kwenye mida ya saa 3:48 usiku na kushitaki kuwa amefanyiwa kitu nyuma na makubaliano yake (kubakwa), hivyo msanii huyo akafunguliwa mashtaka wakati wakiwa kwenye Tour Bus.

Mwanasheria wa msanii huyo amepinga mashataka hayo ya ubakaji na kukataa kitendo alichokifanya na kudai kuwa ni uongo na hivyo sheria ifanye uchunguzi zaidi ili kubaini ukweli.

Nelly amesema kuwa mashtaka hayo ni ya uongo na yupo huru anajiamini kuwa baada ya uchunguzi kila kitu kitajulikana, maneno haya aliyaandika katika kurasa ya twitter.

VIDEO: Rekodi nyingine ya Mtanzania aliyepata udhamini kusoma Harvard University

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement