Tangaza Hapa Ad

Michezo

Klabu imevunja mkataba na staa wa Cameroon baada ya kugundua kuwa ana HIV

on

Moja kati ya habari zinazo-trend kwa siku ya leo August 29 2016 katika soka ni hii ya klabu Al Ittihad Alexandria ya Misri kutangaza kuvunja mkataba na nyota wa kimataifa wa Cameroon Samuel Nlend kutokana na kugundua kuwa nyota huyo ana HIV.

Al Ittihad Alexandria imevunja mkataba na Samuel Nlend mwenye umri wa miaka 21 kutokana na kupimwa kwa nyota huyo na kugundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi, maamuzi hayo yamekuja ikiwa ni siku nne zimepita toka nyota huyo asaini mkataba wa miaka mitatu wa kuichezea klabu hiyo.

Samuel-Nlend

Samuel Nlend

Samuel August 24 2016 alisaini mkataba wa miaka mitatu wa kuichezea klabu ya Al Ittihad Alexandria, Samuel amewahi kuichezea timu ya taifa ya Cameroon mechi tano, hata hivyo hakuna sheria yoyote itakayomzuia staa huyo kupata kibali cha kucheza soka katika nchi nyingine licha ya kugundulika kuwa na virusi vya ukimwi.

GOAL AND HIGHLIGHTS: YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement