Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

AyoTV

Mkemi kuhusu kauli ya Manara “Sisi mpango wa kuishangilia Simba hatuna”

on

Jana afisa habari wa Simba SC Haji Manara alitangaza kuwaomba mashabiki wa Simba kutokwenda uwanja wa Taifa kuwazomea Yanga katika m,chezo wao wa club Bingwa Afrika dhidi ya St Louis ya Ushelisheli, Manara aliwaomba mashabiki wa Simba kuacha dhana ya kushangilia timu za kigeni zinazocheza na watani zao wa jadi Yanga na badala yake wawe wanatanguliza utaifa kwanza.

Yanga anacheza dhidi ya St Louis Jumamosi mchezo wa club Bingwa Afrika wakati Simba anacheza jumapili dhidi ya Gendamarie mchezo wa Kombe la shirikisho barani Afrika, kuelekea mchezo huo tumempata mwanachama na mjumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga Salum Mkemi na kutaka kufahamu mtazamo wake vipi alichokizungumza Manara anakipokeaje? anaweza kuishangilia Simba katika mechi za kimataifa?
“Tunajulikana kama Yanga ni watu wa kimataifa na kesho ndio tunaanza rasmi michuano ya kimataifa naomba waje kwa wingi, nimemsikia Manara akisema mashabiki wa Simba wasiende kuizomea Yanga kwenye mpira lolote linaweza kutokea anayefanya vizuri atashangiliwa na anayefanya vibaya atazomewa ila sisi mpango wa kuishangilia Simba hatuna”>>>Mkemi

VIDEO: Simba imetangaza kumpeleka Haruna Niyonzima India

Soma na hizi

Tupia Comments