Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Mix

PICHA 3: Baraka Da Prince alivyomtembelea Tundu Lissu hospitali

on

Mwishoni wa mwaka 2017 Mbunge wa Singida Mashariki kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu aliripotiwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake Dodoma.

Lissu baada ya shambulio hilo alipatiwa matibabu ya awali na baadae kupelekwa Nairobi kwa matibabu zaidi na kuondolewa kwa risasi mwilini mwake, Lissu akiwa Nairobi Kenya tumeona watu mbalimbali kama makamu wa Rais Mama Samia Suluhu akienda kumjulia hali.

Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi nae alikwenda kumuona na viongozi mbalimbali wa kisiasa, muimbaji wa Bongo fleva Baraka Da Prince leo zimeonekana picha mtandaoni Baraka akiwa Nairobi hospitali akimjulia hali Lissu, inawezekana Baraka Da Prince akawa ndio msanii wa kwa za kufanya hivyo.

VIDEO: Tundu Lissu amtumia salamu Rais Magufuli (KAMA ILIVYOTUMWA)

Soma na hizi

Tupia Comments