Tangaza Hapa Ad

Michezo

Kauli ya Mkhitaryan kuhusu kupewa nafasi ndogo na Mourinho

on

Kiungo wa kimataifa wa Armenia aliyejiunga na Man United msimu huu akitokea Borussia Dortmund ya Ujerumani Henrikh Mkhitaryan amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu kutopata nafasi ya kutosha kuitumikia Man United.

Mkhitaryan amefunguka wakati alipoteuliwa kuwa balozi wa UNICEF kwa nchi yake ya Armenia, kuwa kutopata nafasi kubwa ya kucheza katika kikosi cha Man United hakuvunji ndoto zake za kuendelea kuitumikia Man United.

henrikh-mkhitaryan-714361

“Ni kweli nimekuwa nikipata nafasi ndogo ya kucheza Man United lakini sitokata tamaa, ilichukua muda mrefu kupata nafasi ya kujiunga na Man United, hivyo hakuna kitakachonizuia kutimiza ndoto zangu”

Mkhitaryan alijiunga Man United mwaka huu katika dirisha kubwa la usajli kwa dau la pound milioni 26 akitokea Borussia Dortmund ya Ujerumani, lakini amekuwa hapati nafasi kubwa ya kucheza chini ya Jose Mourinho.

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement