Tangaza Hapa Ad

Michezo

VIDEO: Tukio linaloweza kumfanya Ibrahimovic asirudi uwanjani msimu huu

on

Man United ni miongoni mwa timu zilizochezwa mchezo wake wa marudiano wa robo fainali ya UEFA Europa League dhidi ya Anderletch usiku wa April 20 2017 katika uwanja wake wa Old Trafford, Man United walicheza game hiyo na kukutana na upinzani mkubwa uliyopelekea game yao kuongezwa dakika 120.

Man United wamefanikiwa kuondoka na ushindi wa magoli 2-1 magoli ambayo yalifungwa na Mkhitaryan dakika ya 10 na Marcus Rashford dakika ya 107 wakati goli pekee la Anderletch lilifungwa na Hanni dakika ya 32, hivyo Man United kuingia hatua ya nusu fainali kwa aggregate ya magoli ya 3-2.


Hata hivyo Man United wamepata ushindi uliyoambatana na pigo kwa mshambuliaji wao tegemeo Zlatan Ibrahimovic kuumia goti la kulia  na kutolewa dakika ya 91, hivyo kuumia huko kuna hofu kubwa kuwa Zlatan inawezekana akamaliza msimu huu akiwa nje ya uwanja licha ya kuwa haijathibitika bado.


VIDEO: Game haikuoneshwa Yanga vs MC Alger, nimeyanasa matukio na goli la Yanga FT 1-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement