Biko


Tangaza Hapa Ad

AyoTV

Simon Msuva amerudi Tanzania leo, alichozungumza kipo hapa

on

Alhamisi ya January 5 2018 mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa katika club ya Difaa El Jadid ya Morocco Simon Msuva aliwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere Dar es Salaam akitokea Morocco kwa ajili ya Mapumziko mafupi.

Msuva amewasili asubuhi ya leo baada ya kuichezea timu yake ya Difaa El Jadid michezo 14 ya round ya kwanza kati ya 15 ya Ligi Kuu Morocco, AyoTV ilikuwepo Aiport kwa ajili ya kuzungumza nae baada ya kurudi Tanzania.

 

Simon Msuva kwa sasa atakuwa Tanzania kwa mapumziko ya wiki moja na nusu baada ya Ligi Kuu Morocco kusimama kutokana na round ya kwanza kukamilika lakini pia kupisha michuano ya CHAN inayofanyika nchini humo, kwa upande wa Ligi Kuu Morocco itaendelea mwezi February 2018.

Kitu Msuva kaandika baada ya kusikia Mahadhi kapiga magoti kuomba msamaha

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement