Tangaza Hapa Ad

AyoTV

“Kuna haja ya mimi kurudi kuwa Rais wa TFF” Fredrick Mwakalebela

on

Jina la Fredrick Mwakalebela sio jina geni kwa wapenzi wa mchezo wa mpira wa miguu Tanzania, kama utakuwa unakumbuka vizuri Fredrick Mwakalebela alikuwa katibu Mkuu wa zamani wa shirikisho la soka Tanzania TFF chini ya utawala wa Rais wa wakati huo Leodger Tenga.

Fredrick Mwakalebela ni miongoni mwa wagombea sita wa nafasi za Urais wa shirikisho la soka Tanzania TFF watakaopigiwa kura katika uchaguzi mkuu wa TFF utakaofanyika katika ukumbi wa St Gasper mjini Dodoma kesho August 12 2017, Mwakalebela ametaja sababu zake kwa nini achaguliwe kuwa Rais wa TFF.

“Kuna changamoto kubwa inayotukabili katika timu zetu za taifa za vijana, wanawake na wanaume, hapo nyuma zilikuwa zinafanya vizuri kama utakumbuka hapo nyuma nikiwa kama katibu Mkuu, tuliwahi kuingia katika fainali za CHAN timu ya wakubwa tukashinda Ubingwa wa Copa Cocacola Brazil”

“Pia tuliingia katika fainali za michuano ya mataifa ya Afrika kwa wanawake Twiga Stars kitu ambacho, hapa katikati tumeshindwa kuingia katika fainali zozote kwa hiyo naona kuna haja ya mimi kuwa Rais wa Shirikisho ili kuweka mbinu mbadala, kwanza watu kuipenda timu yao ya taifa”

Zaidi tazama sera za Mwakalebela hapa katika video hii

VIDEO: Ushindi wa Simba vs Rayon Sports, Simba Day 8 2017 Full Time 1-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement