Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Taarifa rasmi kutoka Ubelgiji, Samatta atafanyiwa upasuaji

on

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania anayecheza soka la kulipwa katika club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta siku ya Jumamosi ya November 4 2017 katika uwanja wao wa Luminus Arena alikuwa uwanjani kuitumikia Genk.

Samatta aliichezea KRC Genk katika mchezo wa Ligi Kuu Ubelgiji dhidi ya Lokeren mchezo ambao ulimalizika kwa sare tasa (0-0) lakini nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta ambaye alikuwa akiongoza safu ya ushambuliaji ya Genk alishindwa kumaliza dakika 90.

Mbwana Samatta alishindwa kumaliza dakika 90 na kuishia kucheza kwa dakika 40 za mwanzo kufuatia kuumia goti la kulia, hivyo nafasi yake ikachukuliwa na mgiriki Nikolaos Karelis lakini baada ya hapo Samatta alifanyiwa vipimo na amegundulika kuwa jeraha lake litamuweka nje ya uwanja hadi kipindi cha majira ya baridi.

Azam FC imetangaza kumuacha staa wake wa kimataifa

Soma na hizi

Tupia Comments