Tangaza Hapa Ad

Michezo

Rooney kaachwa katika kikosi cha Man United kitakachocheza na Feyenoord

on

Nahodha wa Man United Wayne Rooney ameachwa katika kikosi cha Man United kilichosafiri kuelekea Uholanzi kucheza mchezo wake wa kwanza wa Europa League dhidi ya Feyenoord, Jose Mourinho amesafiri na kikosi cha wachezaji 20.

Stori kutoka katika tovuti rasmi ya Man United inaeleza Man United kusafiri kwenda Uholanzi kwa ajili ya mchezo na Feyenoord na wachezaji 20 tu ikiwa imewaacha wachezaji kama Antonio Valencia, Jesse Lingard na Wayne Rooney licha ya kuwa walifanya mazoezi na timu asubuhi.

manchester-united-training-session-1

Hakuna sababu rasmi iliyotolewa kuachwa kwa nahodha huyo lakini kiungo Henrikh Mkhitaryan nae ameshindwa kufanya mazoezi na timu kutokana na kuuguza jeraha lake la mguu na Phil Jones hakufanya mazoezi na timu.

ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement