Tangaza Hapa Ad

Featured

Good News iliyothibitishwa na SportPesa kuingia Italia

on

Kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa imetangaza rasmi kuwa imefanikiwa kupata hisa za umiliki wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya RCS ya Italia ambayo inamilikiwa na kampuni mama ya RCS Media Group.
Shughuli za sasa za uendeshaji za kampuni hiyo zimekuwa zikifanywa chini ya usimamizi wa nembo ya GazzaBet ya Italia ikiwa ni miaka mitatu sasa ambapo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika soko la michezo ya kubashiri la Italia.

Mwenyekiti mteule wa Bodi ya SportPesa Italia Adam Beighton amezungumzia kuhusiana na good news kampuni ya SportPesa kuingia Italia ikiwa ni muendelezo wa ukuaji wa kampuni.

“Hii ni hatua nyingine kubwa katika harakati za kuendelea kuifanya SportPesa kuwa kampuni kubwa duniani. Kupata hisa kwenye kampuni ya michezo ya kubashiri ya RCS kutawezesha kampuni kukua kwa kasi nchini Italia na itatoa fursa mpya kwetu kutangaza utamaduni wetu kama SportPesa kwa wateja wetu wa sasa na wa baadae” >>> Adam Beighton

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa SportPesa Tanzania Pavel Slavkov alizungumzia pia good news hiyo kwa kampuni yao kuingia Italia

“SportPesa ina furaha kubwa kutanua wigo wake kibiashara katika nchi ya Italia ambayo imekuwa ni soko kubwa la michezo ya kubashiri barani Ulaya. Kuiongeza Italia kwenye orodha yake ya utendaji ni mafanikio makubwa huku tukitazamia kuboresha huduma kwa wateja wetu waliomo nchini humo na kuzifanya kuwa za kiwango cha daraja la juu zaidi” >>> Pavel Slavkov

Kwa sasa RCS Media Group wataendelea kuwa wamiliki wa hisa wa kampuni hiyo kwa asilimia chache huku wakiwa na shauku kubwa ya kuona jinsi ambavyo fursa hiyo itatanua wigo wa kampuni hiyo kibiashara.

VIDEO: Taifa Stars ilivyoambulia sare ya 1-1 vs Rwanda CCM Kirumba

Tupia Comments

Advertisement