DSTV


Tangaza Hapa Ad

AyoTV

Uzalendo Kwanza mkoa wa Pwani, Steve Nyerere kapewa nyumba

on

Timu ya wasanii na wachezaji wa zamani wanaounda Kundi la Uzalendo Kwanza lilitembelea Mkoa wa Pwani wilaya ya Kibaha Mjini kijiji cha Kwala kwa ajili ya kuangalia eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu mradi unaosimamiwa na VIGUTA.

Uzalendo Kwanza wakiwa mkoani Pwani katika kijiji cha Kwala CEO wa VIGUTA Salmin Dauda alimpa zawadi ya nyumba yenye thamani ya Tsh milioni 20 mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza Steve Nyerere kutokana na kuwa muasisi wa Uzalendo Kwanza.

Steve Nyerere akikabidhiwa hati ya nyumba na mbunge viti maalum Hawa Mchafu ambaye alikuwa mgeni rasmi.

Hata hivyo CEO wa VIGUTA Dr Salmin alionesha eneo la hekari 50 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za wasanii na wachezaji wa zamani wanaounda umoja wa Uzalendo Kwanza, nyumba ambazo watajengewa kwa mujibu wa vipato vyao na gharama nafuu, eneo lipo karibu na bandari kavu.

Ayo TV MAGAZETI: Jela miaka 30 kwa wizi wa simu, Afunguka mazito

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement