DSTV

Tangaza Hapa Ad

Michezo

Taifa Stars imepata sare ya sita chini ya kocha Mayanga leo

on

Jumamosi ya October 7 2017 timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ilicheza game yake ya kimataifa ya kirafiki iliyopo katika kalenda ya FIFA dhidi ya timu ya taifa ya Malawi uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Malawi unakuwa ni mchezo wa 13 chini ya kocha wao Salum Mayanga, wakiwa wamefungwa mchezo mmoja pekee dhidi ya Zambia katika michuano ya COSAFA na wametoka sare game sita na kushinda game sita.

Mbwana Samatta akitolewa kupata matibabu baada ya kuumia

Hivyo game yao kumalizika kwa sare ya 1-1 dhidi ya Malawi inamfanya kocha Mayanga kufikisha sare ya sita toka aaanze kuitumikia Taifa Stars, Ngambi Robert ndio aliifungia Malawi goli la uongozi dakika ya 35 lakini Simon Msuva akaisawazishia Taifa Stars dakika 57.

Baada ya game kocha mkuu wa timu ya taifa ya Malawi raia wa Ubelgiji Ron van Geneugden ameeleza kuwa na mashaka na goli la Taifa Stars na kuoneshwa kutoridhishwa na muamuzi Israel Nkongo, kwa upande wa Taifa Stars walilazimika kumaliza game wakiwa tisa uwanjani kutokana na Erasto Nyoni na Mzamiru Yassin kuoneshwa kadi nyekundu.

KITU SAMATTA KAONGEA KABLA YA KUCHEZA NA MALAWI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement