Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Zawadi atakayopewa Miss Afrika 2016 kesho, Tanzania inawakilishwa na Julitha Kabette

on

Muwakilishi wa Tanzania katika shindano la Miss Afrika 2016,  Julitha Kabette, kesho Jumamosi ya November 26 atapanda jukwaani na washiriki wengine 18 kuwania taji la Miss Afrika 2016 nchini Nigeria.
Mashindano hayo yatafanyika Nigeria katika jimbo la Cross River, mjini Calabar mshindi wa kwanza atapewa zawadi ya dola za Kimarekani 25,000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 5o pamoja na gari jipya.
img-20161125-wa0065
Mshindi  wa pili wa shindano la Miss Afrika 2016 atapata zawadi ya dola za Kimarekani 15,000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 30 na mshindi wa tatu  atapata dola 10,000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 20, Julitha Kabette amepata nafasi ya kushiriki mashindano hayo baada ya kuchaguliwa na kampuni ya Millen Magese  Group (MMG).
VIDEO: OnAIR: Miss Africa Tanzania 2016 Julitha Kabette na Millard Ayo 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement