Tangaza Hapa Ad

Michezo

Maofisa TFF wamefikishwa mahakamani leo Nov 9 2016

on

Baada ya headlines za muda mrefu na tuhuma za baadhi ya viongozi wa shirikisho la soka Tanzania TFF kudaiwa kuomba rushwa ili waweze kupanga matokeo ya mechi za Ligi daraja la kwanza ili wa wapande Ligi Kuu.

Leo November 9 2016 Taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa TAKUKURU wamekamilisha uchunguzi wao na kuwafikisha mahakamani maofisa wawili wa TFF Juma Matandika ambaye ni msaidizi wa Rais wa TFF Jamal Malinzi na  Martine Chacha.

chacha

Martine Chacha

Matandika na Chacha wamefikishwa mahakama ya Kisutu kwa tuhuma za kuomba rushwa ya Tsh milioni 25 kutoka timu ya Geita Gold ili waisaidie kupanda  Ligi Kuu kutoka Ligi daraja la kwanza.

matandika

Juma Matandika

Kwa pamoja Matandika na Chacha wamekana mashtaka na wapo nje kwa dhamana ya Tsh milioni 5 kila mmoja na kesi yao imeahirishwa hadi November 30, wawili hao wanadaiwa kutenda kosa hilo February 4 2016 katika ofisi za TFF.

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement