Tangaza Hapa Ad

Michezo

PICHA: Yanga wachukua point tatu na goli tatu dhidi ya Mbao FC leo Oct 30

on

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu soka Tanzania bara klabu ya Dar es Salaam Young Africans leo October 30 wamerudi dimbani kucheza mchezo wao 12 wa Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu wa 2016/2017, Yanga leo wamecheza kocha wao Hans van Pluijm karejea katika benchi baada ya kukubali kufuta mawazo ya kujiuzulu.

dsc_0237

Yanga leo wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-0, magoli ya Yanga yakifungwa na beki wao Vincent Bossou dakika ya 49 na goli la pili kipa wa Mbao FC Emmanuel Mseja alijifunga kwa kushindwa kuzuia mpira wa kurusha wa Mbuyu Twite dakika ya 56, Amissi Tambwe akaendelea kucheka na nyavu kwa kupachika goli la tatu dakika ya 75.

dsc_0184

Mbao FC hawakuwa rahisi kupoteza mchezo kama ambavyo unaweza kuhisi ni wepesi kutokana na stahili iliyopandisha Ligi Kuu, waliweza kudhibiti safu ya Yanga isipate goli wala kufanya mashambulizi ya hatari katika kipindi cha kwanza hadi dakika nne baada ya kipindi cha pili amapo Yanga waliongeza mashambulizi yalioleta presha na kuzaa goli.

dsc_0237

dsc_0195

dsc_0216

dsc_0152

Matokeo ya mechi za VPL zilizochezwa leo Jumapili ya October 30 2016. pic.twitter.com/oGMWhxSXIf

— millard ayo (@millardayo) October 30, 2016

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement