DSTV

Tangaza Hapa Ad

Michezo

Matokeo ya VPL September 30, Yanga imelazimishwa sare ya tatu leo

on

Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2017/2018 imeendelea tena leo Jumamosi ya September 30 2017 kwa michezo 7 kuchezwa katika viwanja mbalimbali, Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara club ya Dar es Salaam Young Africans walicheza dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Uhuru.

Mchezo wa Yanga dhidi ya Mbitwa Sugar ulikuwa ni mchezo wa tano kwa Yanga wa Ligi msimu wa 2017/2018 lakini wameambulia sare tasa (0-0), hivyo kujikuta wakiambulia jumla ya point 8 katika michezo yao mitano ya Ligi Kuu msimu huu.

Hadi sasa Yanga wanakuwa wamecheza michezo mitano na kuambulia ushindi michezo miwili pekee, huku michezo mitatu wakitoka sare, kwa upande wa Mtibwa Sugar wao wanafikisha jumla ya point 11 msimu huu wakiwa wamecheza michezo mitano, ushindi michezo mitatu na sare game 2.

Matokeo ya mechi nyingine za VPL zilizochezwa September 30 2017

  • Singida United 1-1 Azam FC
  • Ndanda FC 2-1 Lipuli FC
  • Majimaji FC 0-0 Kagera Sugar
  • Mwadui FC 2-2Mbeya City
  • Mbao FC 1-1 Prisons
  • Ruvu Shooting 1-1 Njombe Mji

MAGOLI YOTE: Mbao FC vs Simba FC September 21 Mwanza (2-2)

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement