Biko Ad
CRDB Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Matokeo ya game za Champions League Dec 5, timu zilizofuzu 16 bora

on

Game nane za hatua ya makundi ya michuano ya club Bingwa Ulaya msimu wa 2017/2018 iliendelea usiku wa December 5 2017, hizo zilikuwa ni game za kukamilisha hatua ya Makundi ya michuano ya UEFA Champions League kwa makundi manne ya mwanzo. Club ya Atletico Madrid ambao ni miongoni mwa vilabu ambavyo vimekuwa vikileta ushindani mkubwa katika michuano hiyo, kwa msimu huu wameshindwa kutinga hatua ya 16 bora ya michuano hiyo baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Chelsea, hivyo sasa Atletico anaungana na baadhi ya vilabu kuiga michuano ya Champions League msimu huu. Goli la kujifunga la Stefan Savic dakika ya 75 ndio liliondoa matumaini ya Atletico Madrid kupambana kusonga mbele walau dhidi ya Chelsea walau kwa kushindanishwa kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, dakika ya 56 Saul Niguez ndio alileta furaha kwa Atletico Madrid kwa kufunga goli la uongozi. Michuano ya UEFA Champions League itaendelea Jumatano ya December 6 kwa michezo nane kuchezwa lakini hizi ndio timu zilizotangulia kuingia hatua ya 16, Roma, Chelsea, PSG, Bayern Munich, Barcelona, Juventus, Man United na Basel.

VIDEO: Atayofanya Mo Dewji kwa Simba ndani ya mwaka mmoja

Soma na hizi

Tupia Comments