Biko


Tangaza Hapa Ad

Michezo

Lipuli FC imelinda rekodi yao uwanja wa Uhuru dhidi ya Simba leo

on

Siku moja baada ya Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara club ya Dar es Salaam Young Africans kucheza game yao ya round ya 11 ya Ligi Kuu katika uwanja wa Chamazi na kuambulia sare ya 1-1 dhidi ya Prisons, leo November 26 ilikuwa ni zamu ya watani zao Simba kuwakaribisha Lipuli FC katika uwanja wa Uhuru.

Simba walikuwa wenyeji wa Lipuli FC katika uwanja wa Uhuru lakini uwepo wa Lipuli katika nafasi za chini katika msimamo wa Ligi Kuu haukuifanya kuwa timu dhaifu mbele ya Simba wanaoongoza msimamo wa Ligi, game hiyo imechezwa uwanja wa Uhuru na kumalizika kwa sare ya 1-1.

Lipuli FC licha ya kuanza kuruhusu goli dakika ya 14 lililofungwa na Mwinyi Kazimoto, ilichukua dakika 4 mbele Asante Kwasi kusawazisha goli hilo na kulinda rekodi yao ya kutofungwa na Simba na Yanga katika uwanja wa Uhuru msimu huu, ambapo game yao dhidi ya Yanga ilikuwa   1-1.

Sare ya 1-1 imeifanya Simba kuendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara unaoshirikisha timu 16 kwa kufikisha jumla ya point 23, wakifuatiwa na Azam FC wenye point 22, Lipuli FC kutokana na kuvuna point moja leo dhidi ya Simba bado wanaendelea kuwa nafasi ya 7 kwa kufikisha jumla ya point 14.

VIDEO: Dakika 2 za Yanga walivyonusurika vs Prisons Full Time (1-1)

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement