Biko


Tangaza Hapa Ad

Michezo

Jamaa aliye nyuma ya mafanikio ya Cristiano Ronaldo

on

Kwenye maisha kila mtu ana mtu ambaye amewahi kumsaidia kufikia mahali alipo. Inawezekana ni katika mafanikio au kutoka hatua moja kwenda nyingine ya kimaendeleo. Yawezekana watu wengi hawajawahi kusikia au hawajui kuwa kuna mtu mmoja ambaye alimsaidi staa wa Real Madrid na timu ya Taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo kufikia mahali alipo.

Ronaldo aliwashitua baadhi ya watu wasiomjua rafiki yake Alberto Fantrau hiyo ni baada ya ushindi wa tuzo na kusema: “Ndio mimi ni mchezaji mkubwa kwa sasa lakini mafaniki yangu yote yanatokana na rafiki yangu Alberto asante sana”

Baada ya Ronaldo kusema hivyo watu walianza kuangaliania na kujiuliza Alberto Fabtrau ni nani na ana mchango gani mkubwa kwa Ronaldo kiasi cha kupewa heshima ya kuwa mtu wa kwanza kushukuriwa.

Ronaldo akaeleza “Mimi na Alberto tulicheza pamoja timu za vijana na wakati mascout wa Sporting Lisbon wanakuja kutafuta vipaji kabla ya mchujo wa kutafuta Wachezaji kuanza walisema Mshambuliaji atakayefunga magoli mengi zaidi ya wenzake tutamchukua na kumpeleka katika Academy yetu ya Sporting Lisbon.”

“Siku hiyo timu yetu tulifanikiwa kushinda 3-0, mimi nilifunga goli la kwanza na Alberto akafunga goli la pili kwa kichwa, goli la tatu ndio lilikuwa kila mmoja linamuumiza kichwa ila Alberto alikuwa anacheza pembeni na alipata nafasi ya wazi kufunga.”

“Akiwa face to face na golikipa na akafanikiwa kumpiga chenga golikipa kilichotokea pale alikuwa yeye na goli tupu mimi nikiwa pembeni yake hivyo alikuwa na nafasi ya kufunga goli la tatu na lingekuwa la pili kwa upande wake na angechukuliwa yeye kwenda kwenye academy ya Sporting Lisbon lakini aliamua kunipa pasi mimi nikafunga.”

“Baada ya mechi nilimfuata Alberto na kumuuliza kwa nini aliamua kunipa pasi mimi na sio kufunga mwenyewe lakini jibu alilonipa ni kuwa amenipa pasi mimi nifunge kwa sababu anaamini mimi ni bora kuliko yeye.”

Baada ya pale Ronaldo alipata nafasi katika academy ya Sporting Lisbon lakini Alberto aliachana na soka baada tu ya kucheza ile game. Maisha yake ya sasa ni mazuri kutokana na mafanikio ya Ronaldo. Alberto Fantrau anaishi vizuri na kufaidi mafanikio ya Ronaldo kwa sasa.

Kiasi cha pesa kinachoweza kuvunja mkataba wa Messi na Barcelona

JAMAA ALIE NYUMA YA MAFANIKIO YA CHRISTIANO RONALDO… BONYEZA PLAY HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement