Tangaza Hapa Ad

Michezo

Kauli ya Zlatan aliyoitoa kuhusu kuwa na mpango wa kuondoka Man United

on

Moja kati ya headlines ambazo zimekuwa zikiandikwa kuhusu mshambulaiji wa kimataifa wa Sweden anayeichezea Man United ya England Zlatan Ibrahimovic kuwa kuna uwezekano wa kundoka Man United mwisho wa msimu na kujiunga Ligi Kuu ya Marekani.

Baadhi ya mitandao ya soka imekuwa ikiripotiwa kuwa Zlatan amekuwa hana furaha sana Man United licha ya kuwa amekuwa na mwanzo mzuri na kufanikiwa kuifungia Man United magoli sita, Zlatan amejibu swali kuhusu tetesi hizo akihojiwa na gazeti la Aftonbladet la kwao Sweden.

“Kama nataka kuondoka Premier League? tutaona tu kuhusu najisikiaje kiakili na kimwili ndani ya EPL hilo halina tatizo, nilikuwa na presha kubwa wakati nacheza Paris Saint Germain” 

Zlatan alijiunga na Man United katika dirisha la usajili la mwezi August kama mchezaji huru akitokea klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa, amesaini mkataba wa mwaka mmoja na Man United ambao unamalizika June 2017.

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement