Tangaza Hapa Ad

Vitu saba alivyozungumza waziri Mwakyembe kwa wajumbe kabla ya kumpigia kura Rais TFF


Jumamosi ya August 12 2017 uchaguzi Mkuu wa shirikisho la soka Tanzania TFF unafanyika mjini Dodoma katika ukumbi wa St Gasper , waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Dr Harrison Mwakyembe alikuwa mgeni rasmi katika mkutano wa huo wa TFF.

Waziri Mwakyembe amefungua mkutano na kueleza kuwa kwa mara ya kwanza viongozi wa TFF watakaopigiwa kura na wajumbe wataapishwa kuiheshimu na kuilinda katika ya TFF, hiyo ndio itakuwa mara ya kwanza kwa kiongozi wa TFF kuapishwa.

“Nyie wajumbe 128 wakiwemo wajumbe wapya wa Mkoa wa Songwe mtambue kuwa mmebeba dhamana kubwa ya mchezo wa mpira wa miguu nchini, watendeeni haki watanzania kwa kuwapa viongozi makini viongozi wazuri”>>> Dr Mwakyembe

“Kwa mara ya kwanza viongozi tutakaowapata hapa tutawaapisha hapa mbele ya wapiga kura wao, tunataka tufuate sheria na kanuni kama zilivyo, kama huko ilikuwa inasahaulika leo wataapishwa hapa kiapo cha utii na kiapo cha uadilifu” >>> Dr Mwakyembe

Zaidi unaweza kumsikiliza waziri Mwakyembe hapa

VIDEO: Ushindi wa Simba vs Rayon Sports, Simba Day 8 2017 Full Time 1-0

Soma na hizi

Tupia Comments

On AIRSIKILIZA

Usipitwe na hizi

Advertisement