Biko


Tangaza Hapa Ad

AyoTV

Atayofanya Mo Dewji kwa Simba ndani ya mwaka mmoja

on

Mfanyabiashara Mohammed Dewji ambaye anatajwa kuwa miongoni mwa Mabilionea wa Afrika, leo Jumapili December 3 2017 ametangazwa kuwa mshindi wa zabuni za uwekezaji ndani ya Simba SC kwa asilimia 50.

MO Dewji ametangazwa kuwa mshindi wa zabuni hiyo hivyo katika mfumo wa kisasa wa hisa ambao utakuwa unaiendesha Simba, MO atakuwa na hisa asilimia 50 na hapa kaeleza ni vitu gani ataifanyia Timu hiyo kwenye mwaka wake wa kwanza.

Baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa zabuni, katika hotuba yake MO Dewji ameahidi mambo mbalimbali makubwa kwa timu ya Simba lakini ndani ya mwaka mmoja ameahidi kuwa Simba itakuwa na viwanja viwili vya mazoezi nyasi bandia na nyasi za kawaida, hostel za timu, mgahawa wa kulia wachezaji sambamba nakuahidi kuweka bajeti ya usajili ya Tsh Bilioni 1.

VIDEO: BREAKING: Mo Dewji apata umiliki wa timu ya Simba SC 50%

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement