Michezo

Simba wadhibitiwa na JKT Ruvu Taifa, matokeo ya mechi za VPL za leo August 27

on

Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu wa 2016/2017 round ya pili imeendelea leo August 27 kwa michezo kuchezwa katika viwanja mbalimbali Tanzania, moja kati ya mchezo uliochezwa leo ni pamoja na JKT Ruvu dhidi ya Simba SC ambao walikuwa wenyeji wa mchezo huo uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

IMG_0529

Simba ambao walicheza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara wiki iliyopita na kuondoka na ushindi mnono wa goli 3-1, leo August 27 wameshindwa kutamba dhidi ya JKT Ruvu na matokeo yake wameambulia suluhu ya 0-0, Simba ambao walianza na washambuliaji wake wa wawili wa kimataifa Blagnon na Mavugo licha ya kumuingiza Ajibu hawakufanikiwa kupata matokeo.

IMG_0538

JKT Ruvu msimu huu wameonekana kujidhatiti zaidi na kukataa kupokea kipigo kama walivyokuwa wanasuasua msimu uliopita, kwa matokeo hay0 Simba anakuwa na point nne na magoli matatu wakati JKT Ruvu wanakuwa na point 1 kutokana na kucheza mchezo mmoja tu katika Ligi Kuu msimu.

IMG_0530

Matokeo ya mechi nyingine zilizochezwa August 27 2016

  • Mtibwa Sugar 2-1 Ndanda FC
  • Azam FC 3-0 Majimaji FC
  • Prisons 1-1 Ruvu Shooting
  • Mbao FC 0-1 Mwadui FC
  • Kagera Sugar 0-0 Stand United

ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0

Soma na hizi

Tupia Comments