Tangaza Hapa Ad

Michezo

VIDEO: Wenger kashindwa kuvunja rekodi yake mbovu dhidi ya Jose Mourinho

on

Ligi Kuu England imeendelea tena leo November 19 2016 baada ya mapumziko ya muda mfupi ya kupisha mechi za kimataifa zilizopo katika kalenda ya FIFA, mchezo wa kwanza wa EPL kuchezwa weekend hii ulikuwa ni mchezo kati ya Man United dhidi ya Arsenal.

2913

Mchezo wa Man United dhidi ya Arsenal umechezwa katika dimba la Old Trafford, huo ulikuwa ni mchezo ambao unatazamiwa rekodi ivunjwe au iendelezwa kati ya Mourinho dhidi ya Wenger, kama utakuwa unakumbuka vizuri Arsene Wenger hajawahi kumfunga Jose Mourinho katika EPL.

3500

Licha ya wengi kutarajia historia tofauti mchezo umemalizika kwa sare ya goli 1-1, goli la Man United likifungwa na Juan Mata dakika ya 68 , wakati goli la Arsenal lilifungwa na Oliver Giroud dakika ya 88.

screen-shot-2016-11-19-at-5-35-26-pm

Msimamo wa EPL baada ya matokeo ya mechi ya Man United vs Arsenal

Kwa sasa Jose Mourinho anakuwa kacheza jumla ya mechi 16 dhidi ya Arsene Wenger na kufanikiwa kumfunga mechi 8, sare 7 na amekubali kufungwa katika mchezo mmoja tu wa Ngao ya Hisani.

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement