Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Rais wa TFF ametangaza ujio wa Rais wa FIFA Tanzania kwa mara ya kwanza

on

Rais wa Shirikisho la soka Tanzania TFF Wallace Karia leo Jumanne ya January 2 2018 amekutana na waandishi wa habari na kutangaza ujio wa Rais wa Shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA Gianni Infantino nchini Tanzania.

Wallace Karia

Wallace Karia ametangaza kuwa Infantino atakuja Tanzania na viongozi wengine wa soka kutoka nchi 19 duniani kwa ajili ya kikao cha maendeleo ya soka kitakachofanyika Dar es Salaam February 22 2018 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere.

Gianni Infantino

Wageni wa mkutano huo wa maendeleo ya soka watawasili Dar es Salaam February 20 2018 wakitokea ndani na nje ya bara la Afrika, hii ndio itakuwa mara ya kwanza kwa Rais wa FIFA Gianni Infantino kutembelea Tanzania toka ashike nafasi hiyo.

Niyonzima baada ya Bocco kuipatia ushindi Simba leo

Soma na hizi

Tupia Comments