Tangaza Hapa Ad

Michezo

PICHA 6: Ujenzi ulipofikia wa uwanja wa White Hartlane wa Tottenham

on

Club ya Tottenham Hotspurs ya England leo October 12 2017 imeonesha picha mpya za awamu ya pili ya ukarabati wa uwanja wao mpya wa White Hartlane watakaoanza kuutumia kuanzima msimu wa 2018/19.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Tottenham kwa sasa wanautumia uwanja wa Wembley kama ndio uwanja wao wa nyumbani, hiyo ni baada ya uwanja wao wa White Hartlane kuufunga kwa ajili ya matengenezo na upanuzi wa uwanja huo.

Pamoja na kuwa Tottenham kwa sasa wanatumia uwanja wa Wembley kama wa nyumbani, mashabiki wao wanatamani kuona wakirudi haraka katika uwanja wao wa zamani kutokana na timu yao kutofanya vizuri Wembley, uwanja White Hartlane ukikamilika utakuwa unaingiza mashabiki 61,559.

List ya majina 30 ya wanaowania tuzo ya Ballon d’Or 2017

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement