Tangaza Hapa Ad

Michezo

PSG inajiandaa kutimiza matakwa ya Neymar

on

Club ya Paris Saint Germain ya Ufaransa inajiandaa kutimiza matakwa ya mshambuliaji ghali zaidi duniani waliyomsajili kwa dau la pound milioni 199 kutoka FC Barcelona Neymar, ambapo inataka kumsajili Alex Sanchez wa Arsenal kama alivyopendekeza Neymar.

Neymar na Sanchez

Neymar amekuwa akicheza katika safu ya ushambuliaji kwa kushirikiana na Cavani na Kylian Mbappe lakini stori zinaripotiwa kuwa PSG wanapanga kumsajili Alex Sanchez wa Arsenal ili awe mbadala wa Cavani, usajili ambao unatajwa kuwa ni mapendekezo ya Neymar aliyokuwa amekubaliana na PSG wakati anajiunga nao.

Sanchez ana urafiki wa karibu na Neymar lakini ili Paris Saint Germain wasivunje sheria ya FIFA ya Financial Fair Play watalazimika kumuuza Cavani ili kwenda sawa na hesabu zao za matumizi ya fedha kulingana na kipato chao wanavyoingizaa kwa mujibu wa kanuni za FIFA.

Neymar na Cavani wamewahi kupishana kwa kila mmoja kuhitaji kupata kipaumbele cha upigaji wa faulo na penati.

Cristiano Ronaldo ameuza tuzo yake ya Ballon d’Or

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement