Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

U HEARD: Gari ya Mo Music yachukuliwa na Benki kisa deni

on

U Heard ya XXL leo November 18, 2016 kupitia Clouds FM ipo na stori kuhusu Benki kuchukua gari inayodaiwa ni ya star wa hit single ya Basi Nenda Mo Music. Kwa mujibu wa taarifa ya shuhuda wa tukio hilo amesema kuwa gari hiyo imechukuliwa na Benki wakati Mo Music akiwa Mwanza.

“Sijajua kakamgari ilikuwa yake au ilikuwa ya yule dada aliyekuwa naye kwenye gari, walikuwa kama wanafanya town trip tu ndio jamaa wakatokea wakazuia gari wakashushwa na hao madalali yeye akakimbia ilikuwa ni maeneo ya Cecafa jijini Mwanza. Gari ni aina Verossa. Walikua wanawafatilia kwa nyuma mpaka walivyopaki ndio wakakamatwa.” – Shuhuda 

Soudy Brown amezungumza na aliyedaiwa ni baba yake Mo Music na kueleza kile anachokijua yeye kuhusu taarifa hizo.

“Hiyo sio kweli kitu ambacho nakizungumza kama sio maneno ya pembeni mimi sina taarifa kwamba Mo amekopa gari sasa kama sina hizo taarifa kwahiyo siwezi kujua kama Moshi (Mo Music ) amenyang’anywa gari hapa mimi niko nyumbani kwangu na hakuja na gari hapa” – Baba yake Mo Music

Kuipata full stori bonyeza play hapa chini

 

VIDEO: Ulimiss hii ya Mo Music kufikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kutapeli pesa za Show? Tazama hapa

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement