Tangaza Hapa Ad

Michezo

VIDEO: Wenyeji Gabon wametolewa AFCON 2017, Cameroon na Burkinafaso wakiingia robo fainali

on

Usiku wa January 22 2017 michezo ya mwisho ya Kundi A ya michuano ya mataifa ya Afika 2017 maarufu kama AFCON, ilichezwa kwa muda mmoja kuepusha upangaji wa matokeo kutokana na timu zote nne kuwa na nafasi ya kusonga mbele.

Kwa bahati mbaya AFCON 2017 imeshuhudia mwenyeji Gabon akiaga mashindano hayo kutokana na kulazimishwa sare tasa na timu ya taifa ya Cameroon, hiyo inakuwa sare ya tatu kwa Gabon  ambapo sare hiyo imewafanya wafikishe point tatu na kuambulia kushika nafasi ya tatu huku Guinea Bissau wakishika mkia.

Cameroon na Burkinafaso wao wanatinga moja kwa moja robo fainali ya AFCON kufuatia kufikisha point 5 kila mmoja, Burkinafaso anafuzu baada ya kuifunga Guinea Bissau kwa goli 2-0 katika mchezo wa leo, hivyo wapo nafasi ya kwanza wakiwa na point 5 sawa na Cameroon lakini wanaongoza kwa tofauti ya magoli.


VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement