Tangaza Hapa Ad

Mix

Good News: Hii mpya imetangazwa na Multichoice Tanzania kwa Watanzania

on

Moja ya good news wakati huu kuelekea ligi mbalimbali za soka ulimwenguni ni hii kutoka Kampuni ya Multichoice Tanzania kupitia king’amuzi cha DStv kuzindua kampeni maalum ya Msimu mpya wa Soka ijulikanayo kama ‘Full vyenga Bila Chenga’.

Naambiwa Watanzania kupitia DStv wataweza kushuhudia LIVE mashindano makubwa ya kandanda Duniani zikiwemo Ligi kuu ya Uingereza ‘PL’, na Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga’ na makombe mengine maarufu Duniani.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa msimu mpya wa soka katika ofisi za Multichoice Tanzania Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande  amesema DStv inawahakikishia wateja wake wote kuliona soka katika muonekano bora zaidi na kuweza kufuatilia matangazo yatakayorushwa kwa lugha ya Kiswahili.

>>>”Msimu huu Watanzania, kupitia DStv, siyo tu wataona michuano mbalimbali ya soka ulimwenguni mubashara, bali watayaona katika ubora wa hali ya juu yaani High Definition na zaidi ya yote, tutawapatia fursa Watanzania kufuatilia Ligi Kuu ya Uingereza kwa lugha ya Kiswahili.”

Tupia Comments

Advertisement