Michezo

Beki amekiri ni rahisi kwake kumdhibiti Messi kuliko Mbappe

on

Beki wa kati wa club ya Olympique Lyon ya Ufaransa Marcelo ambaye timu yake wiki hii ilicheza dhidi ya FC Barcelona katika mchezo wa kwanza wa UEFA Champions League hatua ya 16 bora, ameweka wazi kwake ilikuwa changamoto zaidi kucheza dhidi ya Kylian Mbappe kuliko Messi.

Marceloa ameeleza kuwa kwake ilikuwa ngumu zaidi kucheza dhidi ya staa wa Paris Saint Germain Kylian Mbappe ambaye ana kasi sana kuliko changamoto aliyoipata ya kumdhibiti Lionel Messi wakati wa game yao ya 16 bora ya UEFA Champions League msimu wa 2018/2019.

“Nilicheza dhidi ya Mbappe msimu huu ilikuwa kazi ngumu kweli kumkaba, Messi hakucheza vizuri (Jumanne) lakini Mbappe kwa kasi yake, namna anavyojiweka katika nafasi na kucheza na beki ana kwa ana ilikuwa ni ngumu sana kumkaba”>>> Marcelo

Lyon ambao watarudia na FC Barcelona March 13 katika uwanja wa Nou Camp nchini Hispania, wao ndio timu pekee iliyofanikiwa kuifunga PSG katika Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1), hivyo beki wa Brazil anayeichezea Lyon amekiri kuwa ni ngumu kucheza dhidi ya Mbappe na sio Lionel Messi.

Argentina’s forward Lionel Messi congratulates France’s forward Kylian Mbappe (R) at the end of the Russia 2018 World Cup round of 16 football match between France and Argentina at the Kazan Arena in Kazan on June 30, 2018. (Photo by Luis Acosta / AFP) / RESTRICTED TO EDITORIAL USE – NO MOBILE PUSH ALERTS/DOWNLOADS (Photo credit should read LUIS ACOSTA/AFP/Getty Images)

Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera kataja walichozidiwa wachezaji wake na Simba

Soma na hizi

Tupia Comments