Habari za Mastaa

Maneno ya Mwijaku kwa MC Pilipili baada ya kumuoa aliyekuwa mchumba wake

on

Mwijaku ambaye ni mume wa aliyekuwa mpenzi wa Mc Pilipili ambaye ni Nicole Franklyn,  ameamua kumjibu Mc Pilipili kupitia ukurasa wake wa instagram hii ni baada ya Mc Pilipili kuonyesha hisia za kuumizwa na kitendo cha aliyekuwa mpenzi wake kufunga ndoa na muigizaji huyo.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Mwijaku ameandika ujumbe wa kumaliza kile ambacho kinaendelea kumuumiza Mc Pilipili kwa kufunga ndoa na aliyekua mpenzi wake miaka kadhaa iliyopita.

>>>@mcpilipilimalalamiko yako nimeyasikia ,unatakiwa kujua kuwa mapenzi ni kama daladala ukishuka mwingine anapanda pia ulitakiwa ujitathmini kwa nini umemkosa @nicole_franklyn we fikiria tu kwanza unaitwa Pilipili sasa kuna mrembo gani hapa duniani anapenda kuwashwa kutwa kuchaa? (Eti Pilipili)@nicole_franklyn kafata maisha huku kwangu na amependa jina la @mwijaku jina laini na linatamkika vizuri mdomoni”

Pole @mcpilipili maisha ndivyo yalivyo tuache tumalizie hanimuni yetu maneno yako si lolote si chuchote kwetu. NIMEMALIZA 🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾”

MAUMIVU: MC Pilipili alipokuwa MC katika harusi ya mpenzi wake wa zamani

Soma na hizi

Tupia Comments