Habari za Mastaa

Cardi B na Offset kumbe walifunga ndoa ya siri

on

Rapper Cardi B amethibitisha ukweli kuhusiana na tetesi zilizokuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na ndoa yake na Rapper Offset na kusema kuwa ni kweli walifunga ndoa September 20,2017

Cardi B ametumia mtandao wa twitter kuthibitisha ukweli huo ambapo ameandika ujumbe mrefu na kusema kuwa kuna vitu anatamani kuviweka wazi huku vingine kuvifanya siri lakini anaamini  kuolewa na ndoto ya kila msichana na aliamka tu asubuhi na kufanya maamuzi ya kuolewa kwasababu alipendana na Offset na hakutaka kumpoteza.

Kupitia mtandao wa TMZ ulifanikiwa kupata cheti cha ndoa hiyo ikiwa pia  October ,2017 Offset alimvalisha pete ya uchumba Cardi B katika show na taarifa kudai kuwa mwezi huo walikuwa tayari wameshafunga ndoa.

Cardi B pamoja na Offset wanategemea kupata mtoto hivi karibuni ambapo kwa upande wa Cardi B atakuwa mtoto wake wa kwanza huku Offset atakuwa mtoto wake wa pili.

Miaka 9 tokea kifo cha Michael Jackson, kuna haya ya kuyafahamu

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments