PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Habari za Mastaa

Mtuhumiwa wa kwanza wa mauaji ya Rapper XXXtentacion akamatwa

on

Mshtakiwa wa kwanza anayejulikana kwa jina la Dedrick.D. Williams mwenye umri wa miaka 22 anayehusishwa na mauaji ya rappa XXXtentacion  amekamatwa na kutiwa mbaroni na idara ya polisi mjini Florida nchini Marekani.

Polisi wamemkamata mshtakiwa huyo June 20,2018 na kumfungulia mashtaka ya mauaji ambapo sheria ya kifungo hicho ni kufungwa kifungo cha maisha bila kuwa na kipengele cha kupunguziwa adhabu hiyo au kupata msamaha.

Dedrick Williams ni mchoraji tattoo na anajulikana kwa jina maarufu kama Tattooman Chukie kwa upande wa familia ya marehemu XXXtentacion mama mzazi amethibitisha taarifa za kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.

Mashuhuda waliokuwa katika eneo la tukio ambalo rappa XXXtentacion alipigwa risasi June 18,2018  na kufariki katika gari lake, walisema kuwa watuhumiwa walikuwa wanne na mmoja wao alivaa mask nyekundu kuziba uso.

EXCLUSIVE: Aika kaeleza upekee wa style yake ya nywele na sababu kuiweka

Soma na hizi

Tupia Comments