Wafanyakazi wapya katika hospitali ya taifa ya Muhimbili MNH wamelalamikia kutolipwa mishahara kwa miezi minne sasa huku uongozi ukishindwa kuwapa majibu ya ufumbuzi wa tatizo hilo.
Wafanyakazi hao zaidi ya5o waliajiriwa na Hospitali hiyo tangu mwezi wa nane mwaka huu waliliambia Gazeti hili kwa nyakati tofauti hawajalipwa fedha zao tangu walipoajiriwa.
Walilalama kwamba kilichofanyika hadi sasa ni baadhi yao kupewa namba za hundi,lakini wlaipokwenda kuangalia kwenye akaunti zao hawakukuta kitu.
Mkuu wa kitengo cha Uhusiano cha Hospitali hiyo Aminiel Aligaesha alikiri kuwepo kwa hali hiyo na kusema wenye madai ya mishahara ni wafanyakazi 10 tu na wataanza kulipwa mwisho wa mwezi huu.
MWANANCHI
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amewatuhumu vigogo wa Serikali kwa ufisadi wa Dola milioni 600 za Marekani sawa na trilioni1.2 walizotumia katika mradi wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es salaam.
Bomba hilo lililoanza kujengwa mwaka jana litasafirisha gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar ili kuongeza vyanzo vya nishati ya umeme nchini.
Alisema awali kampuni iliyokua ikijenga mradi huo ilisema gharama za ujenzi ilikua trilion1.2 lakini viongozi wakaongeza mara mbili ya fedha hizo kwa manufaa yao binafsi.
“Huu ni ufisadi wa hali ya juu na nitathibitisha maelezo yangu popote nitakapotakiwa kufanya hivyo,inauma sana fedha hizi zitalipwa na Watanzania maskini wakati nusu yake inaingia kwenye mifuko ya vigogo”Alisema Mbowe
HABARILEO
Hali ya hewa imechafuka katika Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa Ngorongoro baada ya Wakurugenzi wanne wa mamlaka hiyo kusimamishwa kazi kwa tuhuma za ubadhirifu wa mabilioni ya fedha.
Taarifa kutoka ndani ya Mamlaka hiyo imesema kuwa Wakurugenzi hao ni Mkaguzi Mkuu wa ndani Elinipendo Mbwambo,Mkurugenzi wa Utalii,Mkurugenzi wa Ulinzi,Mhandisi mkuu na Mkurugenzi wa maendeleo ya jamii ambao walisimamishwa tangu Novemba3 mwaka huu na walikabidhiwa barua zao za kusimamishwa kazi.
Vigogo hao wamesimamishwa baada ya tume iliyoteuliwa na Waziri Hamis Kagasheki kubaini ubadhirifu huo wa fedha uliotokea kwa kipindi cha mwaka2008 hadi 2010.
Miongoni mwa tuhumu zinazowakabili ni pamoja na kujilipa fedha hewa za tiketi za ndefe kwenda nje ya nchi na kuidhinisha malipo makubwa ya fedha bila idhini ya bodi wakati wakijua ni kosa kisheria.
MTANZANIA
Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe amelitaka Bunge libadilishe kanuni zake ili ziruhusu Mawaziri wanaosema uongo wachapwe viboko.
Amesema Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika Chrisptopher Chiza anapaswa kucharazwa bakora kwa kusema uongo bungeni wakati akizungumzia suala la masoko ya wakulima wa kahawa na mahindi.
Alisema katiika kikao cha juzi Chiza alipoulizwa swali alikosa majibu ya uhakika na kuzungumza uongo hivyo kutakiwa kujiuzulu
“Ili iwe fundisho kwa Mawaziri wengine nilitegemea waziri huyu angejiuzulu baada ya kushindwa kujibu ma swali ya msingi kuhusu madai ya wakulima wa pamba wakati mazao yao yanaoza,mvua zinanyesha na hakuna masoko ya uhakika”alisema Filikunjombe.
MTANZANIA
Jeshi la Polisi Wilayani Bunda Mkoani Mara linawashikilia wanawake wawili kwa kosa la mmoja kumtekeleza mtoto wake wa mwaka mmoja kwa kumfungia katika chumba cha rafiki yake kwa muda wa siku saba na kutokomea pasipojulikana.
Mtoto huyo alitekelezwa na mama yake Jackline Bhoke mwenye miaka20 baada ya wiki walirejea na kudai walitoka Mwanza mjini kutafuta maisha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Philipo Kalangi alisema wanawake hao kwa sasa wanashikiliwa na jeshi hilo wakati uchunguzi ukiendelea kujua hatma ya mtoto huyo.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook