Habari za Mastaa

Kilichosababisha Shakira kutaka kuacha muziki

on

Staa maarufu kutokea Colombia Shakira ambaye wengi humuita kiuno bila mfupa kutokana na uchezaji wake amefunguka baada ya kuhairisha ziara yake ya muziki El Dorado World Tour kwa miezi 7 kutokana na matatizo ya sauti aliyopata kwa kipindi hicho.

Hatimaye staa huyo alifanikiwa kufanya show kubwa June 3,2018 mjini Hamburg nchini Ujerumani katika viwanja vya Barclaycard Arenaย ikiwemo na kusumbiliwa na matatizo ya sauti na hata kumlazimu kukaa bila kufanya show yoyote kwa miezi saba na hadi kufikia maamuzi ya kutaka kuachana na kazi hiyo ya sanaa.

Kupitia mahojiano aliyoyafanya na BBC Shakira alieleza kuwa “Mwaka jana ulikua moja kati ya mwaka mbaya sana, ilikua ni zaidi ya tatizo sababu damu zilikuwa zikitoka kwenye mishipa ya koo ilifikia muda nikawa ninahofu kwamba nitashindwa kusimama mbele za watu na kuimba”

Nini amfungukia Nay wa Mitego

Soma na hizi

Tupia Comments