Tangaza Hapa Ad

Mix

PICHA 6: Kutoka kwenye eneo Treni ya abiria kutokea Kigoma ilikopinduka

on

Treni ya abiria ya EXPRESS ikitokea Kigoma kuelekea Dar es salaam leo January 29 2017 imepata ajali maeneo ya Ruvu ndani ya mkoa wa Pwani ikiwa ni kilometa kadhaa kabla ya kufika kwenye jiji la Dar es salaam.

Shuhuda ambaye alikua ndani ya Treni hiyo ameongea na Perfect Crispin kwenye ON POINT ya CloudsFM na kuthibitisha kutokea kwa ajili hiyo akisema Behewa zaidi ya 10 zimepinduka na watu wanaendelea kuokolewa kwa kupitia Madirishani.

Amesema ‘Treni imepata ajali kama kilometa moja kutoka Mto Ruvu, abiria wanazidi kuokolewa na hivi ninavyoongea na wewe hatujui idadi ya waliojeruhiwa wala kufariki ni wangapi‘

millardayo.com na AyoTV inafatilia kwa ukaribu zaidi ili kukupatia kila unachostahili kufahamu.

ULIPITWA? Bonyeza play hapa chini kufahamu njia waliyotumia Wachimbaji 15 waliofukiwa Mgodini Geita kufikisha ujumbe kwamba bado wako hai.

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement