Top Stories

Goodnews: Serikali ya Marekani imekuja na mradi wa Dola Milioni 20,Tanzania

on

Leo November 5, 2018, Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Inmi Patterson na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa Muungano na Mazingira, January Makamba wamezindua mradi utakaogharimu Dola za Kimarekani milioni 20 ili kuboresha usimamizi katika kuhifadhi mazingira.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani nchini, umebainisha kuwa mradi huo utafanyika Ukanda wa Magharibi mwa Tanzania. Mradi huo  wa uhifadhi wa mazingira unafadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) na utatekelezwa kwa ushirikiano wa pamoja na Taasisi ya Jane Goodall (JGI).

Mradi huo mpya unatarijiwa kusaidia watu wa Mikoa ya Kigoma na Katavi, pamoja na serikali za mitaa, katika utekelezaji wa mipango ya matumizi bora ya ardhi na utakaonufaisha vijiji 104.

“Mradi huu wa Uhifadhi wa Mazingira umeundwa kulinda mazingira, pia unasaidia wananchi katika shuhuli za kujikimu kiuchumi na maisha bora kama vile uzalishaji wa kahawa na utalii asili kwa ajili ya watanzania,”amesema Balozi Dkt.Patterson

Marekani imewaonya Raia wake wanaoishi Tanzania juu ya agizo RC Makonda

Soma na hizi

Tupia Comments