Habari za Mastaa

CONFIRMED: Familia ya Jay Z & Beyonce kutua katika ardhi ya Mandela

on

Hii ni officially confirmed kuwa familia ya “Carters” Jay Z pamoja na Beyonce watakanyaga ardhi ya Mandela (Afrika Kusini) December 2,2018 katika tamasha la Global Citizen litakalofanyika katika viwanja vya FNB nchini Afrika Kusini.

Lengo la tamasha hilo ni kutimiza maadhimisho ya miaka 100 ya Rais wa kwanza wa Afrika Kusini Marehemu Nelson Mandela ambaye July 18,2018 ni siku yake ya kuzaliwa ikiwa tamasha hilo ni kukumbuka  maisha yake pamoja na kuenzi alichokifanya aliamini katika watu kufanya kazi pamoja.

Tamasha hilo litahudhuriwa na mastaa wengi watakaofanya show kutokea ndani na nje ya bara la Afrika akiwemo Wizkid(Nigeria), Tiwa Savage(Nigeria), Cassper Nyovest(Afrika Kusini), D’Banj(Nigeria), Ed Sheeran, Pharrel Williams na wengine wengi.

Hatimae Moni na Nai watoka pamoja, wakiri kurudiana

Soma na hizi

Tupia Comments