Tangaza Hapa Ad

Michezo

Dalili kubwa ya George Lwandamina inayoashiria atajiunga na Yanga

on

Taarifa kutoka katika mitandao ya Zambia leo November 7 2016 ni kuhusiana na aliyekuwa kocha mkuu wa Zesco United George Lwandamina kujiuzulu nafasi hiyo ambapo mkataba wake ungemalizika January 2017, kitendo hicho kinadaiwa ni dalilia za kujiunga na Yanga.

Zaidi ya mwezi Lwandamina amekuwa akihusishwa  kujiunga na Yanga kuchukua nafasi ya muholanzi Hans van Pluijm, maamuzi ya Lwandamina kuachia nafasi hiyo yamebarikiwa na uongozi wa Zesco na yamethibitishwa na CEO wa Zesco Justin Mumba na afisa habari wao Katebe Chengo na kusema nafasi yake itarithiwa na msaidizi wake Tenant Chembo hadi mwisho wa msimu.

george-lwandamina

Lwandamina alikuwepo Dar es Salaam October 24 akidaiwa kufanya mazungumzo na viongozi wa Yanga licha ya yeye kukanusha na kusema alikuja kwa biashara zake binafsi, Lwandamina alijiunga na Zesco United 2014 na ameipa mataji  mawili ya Ligi Kuu, Barclay Cup, Charity Shield na ameiongoza timu hiyo 2016 kufika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

CHANZO:lusakatimes.com

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement