PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Top Stories

Mtu na Mpenzi wake wamefariki wakipiga Selfie juu ghorofa

on

Mtu na Mpenzi wake Raia wa Australia wamefariki baada ya kudondoka kutoka kwenye ukuta mrefu wa fukwe maarufu ya Ericeira nchini Ureno walipokuwa wakipiga Selfie.

Taarifa zinasema kuwa Wapenzi hao walidondoka kutoka umbali wa mita 30, na Miili ya yao iliokotwa na msafishaji wa fukwe hiyo asubuhi ya June 11.

Polisi wamesema kuwa wanaamini Wapenzi hao walikosa usawa walipokuwa kwenye ukuta huo na kudondoka chini.

Timu ya waokoaji imeeleza kuwa walikuta simu ya mkononi katika eneo la tukio na kuamini kwamba Wapenzi hao walikuwa wanapiga Selfie na ndipo simu ikadondoka kisha wakajaribu kuiokoa na ndipo walipodondoka chini .

Mpaka sasa Wapenzi hao bado hawajatambuliwa majina yao lakini inakadiriwa kuwa Mwanamke anaweza kuwa na umri wa miaka 30 huku Mwanaume akitazamiwa kuwa na umri wa miaka 40.

Maneno ya Rais Magufuli kwa TB Joshua katika Birthday yake

Soma na hizi

Tupia Comments