Michezo

VIDEO: Kocha wa Yanga amwaga machozi, ashindwa kufanya interview

on

Kocha Mkuu wa Club ya Dar es Salaam Young Africans Mwinyi Zahera ameiongoza timu yake katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons jijini Mbeya na kufanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-1, baada ya mchezo huo kocha wa Yanga Mwinyi Zahera alianza kuzichukua headlines.

Yanga wamepata ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Tanzania Prisons lakini baada ya mchezo Mwinyi Zahera aliwaacha watu midomo wazi wakati wa kufanya mahojiano, kutokana na kushindwa kufanya interview na kuanza kulia ghafla kitu ambacho wengi walishindwa kukielewa inatokana na nini.

Machozi ya Zahera hayahusishwi na ushindi sana kwani wakati anaombwa kufanya interview na Azam TV alikuwa katika hali ya kawaida ila ghafla akaanza kulia na kuondoka huku akishindwa kueleza kinachomliza, magoli ya Yanga katika mchezo huo yamefungwa na Ibrahim Ajib dakika ya 76 na Amissi Tambwe aliyefunga mawili dakika ya 85 na dakika za nyongeza.

Yanga wamepata ushindi huo wakitokea nyuma kwani Tanzania Prisons walikuwa wanaongoza mchezo kwa goli moja lililofungwa mapema na Jumanne Elifadhili kwa penati dakika za nyongeza kabla kwenda mapumziko, Yanga wanaendelea kuongoza Ligi kwa kuwa na point 38 wakifuatiwa na Azam FC wenye point 33 na mchezo mmoja mkononi, Prisons wao wanashika mkia.

MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe

Soma na hizi

Tupia Comments