Michezo

Joey Barton amfananisha Neymar na Kim Kardashian

on

Staa wa soka wa zamani wa club ya QPR na kocha wa Fleetwood Joey Barton amenukuliwa na vyombo vya habari kwa kauli yake ya kueleza kuwa kwenye soka kuna Kim Kardashian pia wa soka.

Neymar

Barton amemtaja Neymar uwezi kumuweka katika level moja na staa wa FC Barcelona Lionel Messi au staa wa Juventus Cristiano Ronaldo kwani wanauwezo mkubwa zaidi yake na wapambanaji.

Barton

“Nafikiri Neymar ni Kim Kardashian wa soka kwani Neymar sio mchezaji bora duniani tumeona hilo katika Kombe la Dunia, hayupo level moja na Ronaldo na Messi kuna wachezaji wengi wamempita”>>>Barton

Barton

Kama humfahamu vizuri Kim Kardashian ni mke wa Rapper Kanye West lakini umaarufu wake mkubwa ulitokana na Reality TV show ya Keeping Up With The Kardashians.

EXCLUSIVE: Licha ya kuwa na pesa na ustaa, hii ndio Sababu inayomfanya Samatta asiringe

Soma na hizi

Tupia Comments