Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Taarifa kutoka Hospitali aliyopo Wastara kuhusu Matibabu yake

on

Siku ya February 10, 2018 imetolewa taarifa na Masoud Kaftany ambaye ni Afisa Habari, Uenezi , Mahusiano katika chama cha Waigizaji  Kinondoni, kuhusu Muigizaji Wastara Juma taarifa hiyo inasema Wastara ameshafanyiwa Vipimo (Operation ) na anaendelea kupatiwa Matibabu.

Muigizaji Wastara ambaye yupo katika Hospitali ya Saifee (Mumbai ) Nchini India anaendelea vizuri na siku hiyo ya jana alitembelewa hospitalini na  Muigizaji wa Bongomovie REGINA KAOLE  ambaye yupo Mumbai nchini India kwa shughuli zake za kikazi.

Wanatasnia na wadau wa filam nchini wanaombwa kuzidi kumuombea Muigizaji huyo Wastara ili apone Haraka na kurejea nchini salama.

WASTARA AMEFIKISHA ZAIDI YA MILION 37 AMSHUKURU JPM, ALIKIBA NA WENGINE

Mpaka leo Wastara yupo nchini, Nini kimemfanya asiondoke?

Soma na hizi

Tupia Comments