Tangaza Hapa Ad

Top Stories

PICHA 15: Rais Magufuli alivyokutana na Jenerali Fan Changlong wa China, Ikulu DSM

on

November 21, 2016 IKULU ya Tanzania imepata ugeni wa kutembelewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni Kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong, ambapo amekutana na kuzungumza na Rais Magufuli.

Viongozi hao wamezungumzia uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya Tanzania na China katika nyanja mbalimbali ikiwemo katika masuala ya ulinzi ambapo Jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) limekuwa na ushirikiano na Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA)

Rais Magufuli amemueleza Jenerali Fan Changlong kuwa Tanzania inathamini ushirikiano huo ambao umechangia kufanikisha juhudi za kuimarisha JWTZ zinazolenga kuwa na Jeshi la Kisasa na vifaa bora.

Dkt. Magufuli amemuomba Jenerali Fan Changlong afikishe salamu na shukrani zake kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping na kumhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na China katika kuimarisha majeshi ya ulinzi na pia katika masuala mengine ya maendeleo ya kijamii.

“Nimefurahishwa na ziara yako hapa nchini kwetu, ujio wako unazidi kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya nchi zetu ulioasisiwa na waasisi wa mataifa haya Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania na Hayati Mwenyekiti Mao Tse-tung wa China.

“Naomba unipelekee salamu zangu kwa Rais Xi Jinping na umwambie kuwa pamoja na kuendeleza uhusiano na ushirikiano wetu katika kuimarisha majeshi pia tunatarajia kuona China inakuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi zetu za maendeleo kwa kujenga viwanda na kushiriki katika miradi mingine ukiwemo ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani Standard Gauge” –Rais Magufuli.

Kwa upande wake Jenerali Fan Changlong amempongeza Rais Magufuli kwa uongozi imara aliouonesha katika Awamu ya Tano na amemhakikishia kuwa China itaendeleza na kuimarisha ushirikiano wake na Tanzania katika masuala ya usalama hasa kuimarisha JWTZ.

Jenerali Fan Changlong amesema Jeshi la Ukombozi la Wananchi wa China na Jeshi la Wananchi Tanzania yana uhusiano wenye manufaa makubwa na kwamba hivi sasa yanafanya uboreshaji utakaoyaimarisha zaidi na kuwa majeshi ya kisasa.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange na Makamanda wa Majeshi wa Tanzania na China.

4

Rais Magufuli akiwa na mgeni wake Fan Changlong, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

7 10 14 25 35 63 121  aeuw  h sut wa46y xfn ya

VIDEO: Dakika 16 za Rais Magufuli akieleza tathmini ya Mwaka mmoja wa Uongozi wake. Tazama hapa

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement